Tanzania: Mkoa wa Lindi

Rudi kwenye Utafiti

Mkoa wa Lindi upo katika nyanda za juu Kusini Mashariki mwa Tanzania, ukipakana na Mkoa wa Morogoro na Ruvuma kwa upande wa Magharibi, Mkoa wa Pwani kwa upande wa Kaskazini, mkoa wa Mtwara kwa upande wa Kusini na Bahari ya Hindi kwa upande wa Mashariki. Mkoa wa Lindi una jumla ya eneo la kilomita za mraba 58,936, ambalo ni takriban ukubwa wa nchi ya Ireland. Karibu robo ya eneo hilo, kilomita za mraba 18,000, ni sehemu ya Hifadhi ya Mbuga ya Selous.

Eneo hili lina msimu mmoja wa mvua kwa mwaka wastani wa kiasi cha mm 150 katika miezi ya Desemba, Januari, Februari, Machi, Aprili, hadi wastani wa kiasi cha mm 20 kwa mwaka wote. Kipimo cha wastani wa joto kipo kati ya kiwango cha chini cha 19 °C hadi 30 °C kwa mwaka mzima.

Kuhusu topografia, mkoa wa Lindi una urefu wa wastani wa mita 475 juu ya usawa wa bahari na vilele vya juu hufika hadi mita 3000. Udongo wa Lindi umetawaliwa zaidi na chenga mawe za mchanga, zilizoainishwa kama “Cambic Arenosols” upande Magharibi mwa mkoa. Upande wa Mashariki upo tofauti kwasababu unajumuisha matabaka ya aina mbali mbali za mchanga , kama Ferric Luvisols, Eutric Gleysols and Chromic Cambisols.

Chanzo: Vegi-Leg

Sanjari na hilo, mkoa wa Lindi unaweza kuwekwa katika maeneo makuu manne ya ikolojia ya kilimo:

  1. Ukanda wa chini wa pwani (0 m–120 m),
  2. Ukanda wa kati wa chini wa pwani  (120 m-750 m),
  3. Tambarare za kati (750 m-850 m) na
  4. Ukanda wa juu (850 m +).

Uzalishaji wa kilimo katika mkoa huu kwa kiasi kikubwa ni wa kutegemea mvua na mazao makuu ya biashara yanayopandwa ni korosho, ufuta, karanga na alizeti. Mazao ya chakula, ambayo ni muhimu katika mfumo wa kujitosheleza wa kilimo, ni pamoja na mihogo na mtama, lakini pia mahindi, mbaazi na kunde.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi za Tanzania za “sensa ya Idadi ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 “, jumla ya wakazi wa mkoa wa Lindi walikuwa takriban 865,000, walio katika wilaya sita (Kilwa, Lindi DC, Lindi MC, Nachingwea, Liwale na Ruangwa) na zaidi ya 80% ya idadi hiyo wanaishi vijijini.

Mkoa wa Lindi una moja ya uwiano wa chini kabisa kati ya watu na eneo la ardhi nchini Tanzania, yani wakazi 12 kwa kilomita moja ya mraba. Kaya zinajishughulisha na kilimo cha kujikimu au kilimo kidogo ili kupata kipato na sehemu kubwa ya chakula kinachotumiwa ndani ya kaya. Mkoa huo unakabiliwa na kiwango kikubwa cha ukosefu wa usalama wa chakula na ni moja wapo ya mikoa yenye ukosefu wa usalama wa chakula nchini Tanzania.

Vegi-Leg inafanyika katika vijiji viwili vya majaribio: Kijiji cha Mitumbati Wilaya ya Nachingwea na kijiji cha Mibure Wilaya ya Ruangwa. Kulingana na hesabu rasmi ya watu, Mitumbati ina watu 4850 wakati Mibure ina watu 3080. Wilaya zote mbili zilizochaguliwa, Ruangwa na Nachingwea, zina tofauti kulingana na mzunguko wa fedha katika kilimo na uwepo wa madini kama malighafi muhimu kwa shughuli za uchimbaji. Wilaya ya Ruangwa inahusika zaidi katika shughuli hizi kuliko wilaya ya Nachingwea.

Ramani ya vijiji vya Mradi katika Mkoa wa Lindi