Mfumo wa uchambuzi wa mradi wa Vegi-Leg

Ili kukabiliana na aina tofauti za utapiamlo, mradi wa Vegi-Leg utatengeneza njia za kibunifu kwa lengo la jumla la kuboresha hali ya lishe ya watu nchini Msumbiji na Tanzania kwa kuboresha usindikaji wa chakula na mbinu za uhifadhi wa chakula. Italenga kutatua changamoto kwa kutumia njia shirikishi yenye kujumuisha wadau mbalimbali kwa kutumia minyororo ya thamani ya chakula kama mfumo wa uchambuzi (Kielelezo namba 1). Kwa kufanya hivyo, mradi unazingatia maeneo matano ya muhimu kwa uchambuzi zaidi na uingiliaji kati.

Maeneo ya uchunguzi kifani

Tanzania
Msumbiji

Kielelezo namba 1: Muundo wa Vegi-Leg na maeneo ya kuzingatia kwa uingiliaji kati wa 2018-2021

Eneo zingatizi 1: Minyororo ya thamani ya chakula

Mradi huu utachambua uhusiano na mwingiliano wa minyororo ya thamani ya mbaazi na mboga asilia za Kiafrika  katika maeneo ya majaribio yaliyochaguliwa pamoja na maeneo mengine kwa upana. Sehemu kutanishi zita ainishwa ili kurahisisha utekelezwaji wa mbinu endelevu zaidi baina ya minyororo ya thamani ya Mbaazi na mboga asilia za Kiafrika, msisitizo ukiwekwa  katika teknolojia ya usindikaji na uhifadhi wa chakula. Mradi huu utazingatia uchambuzi ufuatao:

 • Kufanya utafiti wa uanishaji wa wigo wa maudhui ya mradi kwa kila nchi ili kubaini na kufafanua minyororo ya thamani iliyopo ya mazao yaliyo ainishwa na kufafanua hali ya sasa ya usalama wa chakula

 • Uchambuzi wa awali (tafiti za kaya) kutambua vigezo vya kijamii na kiuchumi, muundo wa uzalishaji, mifumo ya usindikaji na matumizi. Kwa kuongezea, hali ya lishe itatathminiwa kwa kutumia vipimo vya uzito, urefu pamoja na mzunguko wa mkono na kwa kupima viwango vya damu vya wahusika wa utafiti.

 • Tathmini ya mifumo ya uzalishaji wa rasilimali asili na uchambuzi wa kiwango cha hali ya virutubishi vya mbaazi na mboga za kiasili za Kiafrika.

 • Kuorodhesha njia za asili za usindikaji na uhifadhi sambamba na kupima upotezaji wa chakula kwa kiasi na ubora baada ya mavuno pamoja na mahitaji ya nishati kwa ajili ya usindikaji endelevu.

Eneo zingatizi 2: ushiriki wa wadau, udhibiti na tathmini

Vegi-leg inahusisha makundi yote muhimu ya wadau waliopo katika mradi huu ili kuhakikisha utekelezaji mzuri, uendelevu baada ya mradi kwisha na matokeo ya kisayansi ya hali ya juu. Mradi utazingatia shughuli zifuatazo:

 • Kufafanua makundi ya wadau muhimu ikiwa ni pamoja na makundi madogo madogo.

 • Kujadili maswali yote kama mkutano wa wataalamu, kwa kiwango cha kisayansi

 • Kutengeneza kikundi cha watekelezaji katika ngazi ya kijiji kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za kijamii zilizo pangwa na mawasiliano na jamii.

 • Kushirikisha watunga sera na watoa maamuzi wengine katika ngazi tofauti ili kushawishi mipango ya sera katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kitaifa

Eneo zingatizi 3: Utengenezaji wa mbinu na tahmini

Mradi huu utabaini na kukuza teknolojia bora na za kibunifu za usindikaji ili kutoa bidhaa zakusindika zenye maisha marefu ili kuhakikisha upatikanaji wa kudumu wa vyakula vyenye virutubishi na kipato kinachoweza kupatikana. Teknolojia bunifu zinazoendana na mfumo wa maisha ya vijijini zitazingatiwa na mradi. Mradi utatilia mkazo shughuli zifuatazo:

 • Utengenezaji shirikishi na majaribio ya mbinu za asilia za usindikaji wa mbaazi na mboga za majani za asili za Kiafrika zenye tija(teknolojia ya usindikaji yenye kutunza virutubishi)

 • Uchambuzi wa mabadiliko katika virutubishi vidogo na hadhi ya protini kabla na baada ya usindikaji (Mfano: kukausha kwa jua kuliko boreshwa)

 • Uchambuzi wa uwezo wa soko na nishati wa teknolojia bora za usindikaji kulingana na bidhaa husika

 • Utengenezaji wa teknolojia wenye kuhusisha wadau mbalimbali – Uanzishwaji wa biashara ndogondogo/za kati za usindikaji.

Eneo zingatizi 4: Ukuzaji uwezo-Mafunzo na Elimu

Vegi-Leg itatengeneza na kutekeleza mpango mahsusi wa kukuza uwezo katika ngazi ya wananchi wa kawaida, ukijumuisha njia za wazi za maboresho. Maswala muhimu yatakayoshughulikiwa ni (1) kuongeza ufahamu wa vyakula vilivyo vilivyosindikwa na kusheheni virutubishi; (2) kuongeza maarifa juu ya uandaaji na usindikaji bila kupoteza virutubishi kwa ngazi ya kaya, (3) kuboresha mikakati mahsusi ili kukabiliana na uhaba wa vyakula vilivyo sheheni virutubishi hasa wakati wa kiangazi. Mradi utazingatia shughuli zifuatazo.

 • Elimu na uwezeshaji hususan kwa wanawake katika ngazi ya jamii na mkoa.

 • Mafunzo juu ya mbinu za usindikaji katika ngazi ya jamii na mkoa.

Eneo zingatizi 5: Uhamishaji wa Maarifa, Utekelezaji na Usambazaji

Vegi-Leg itahakikisha inahamisha na kusambaza matokeo ya Vegi-Leg kwa ufanisi mkubwa kwenda kwenye vitendo (kwanza miongoni mwa washiriki wa mradi na pili kwa ngazi zote za wadau mbali mbali). Mradi utazingatia shughuli zifuatazo:

 • Vipengele vyote vya mradi vitatekelezwa katika ngazi ya kijiji na ya mkoa

 • Utekelezaji wa matokeo muhimu ya mradi ili kuboresha programu ya elimu ya vyuo vikuu (Hasa shahada ya kwanza)

 • Utekelezaji wa sera unalenga mipango ya sera ya mkoa na ya kitaifa.

Kielelezo namba 2: Maeneo ya majaribio ya Vegi-Leg