Mradi wa Vegi-leg unalenga kuboresha hali ya lishe sehemu za vijini nchini Tanzania na Msumbiji kupitia teknolojia bunifu ya usindikaji

Usalama wa chakula na lishe bado ni moja ya changamoto kubwa inayo kabili idadi ya watu inayokua kwa kasi Barani Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Katika nchi Hizi mbili za Mashariki mwa Afrika Tanzania na Msumbiji hali ya lishe imeboreshwa kidogo katika muongo mmoja uliopita licha ya viwango vya juu vya ukuaji wa uchumi.

Mradi wa Vegi-Leg unalenga kuboresha hali ya lishe ya wenyeji nchini Tanzania na Msumbiji kwa kuboresha usindikaji baada ya mavuno wa vyakula vitokanavyo na mimea vilivyo sheheni virutubisho vingi kuongeza upatikanaji wa chakula wa kudumu. Mradi huo utajikita katika vyakula vitokanavyo na mimea vyenye virutubisho vingi hususan protini ya hali ya juu (asidi muhimu ya amino), virutubishi vidogo vidogo (chuma) na vimeng’enywa vya pili vya mmea (pro-vitamini A carotenoids) hivyo kupelekea mradi huu kuchagua mbaazi (Cajanus cajan) na mboga asilia za Kiafrika kwa ajili ya usindikaji. Katika muundo shirikishi wa majaribio, Vegi-Leg itachunguza minyororo ya thamani ya chakula na kubuni mbinu mpya za usindikaji au kuboresha zilizopo ili kuhakikisha upatikanaji wa vyakula vilivyo sheheni virutubisho vitokanavyo na mimea wakati wa msimu wa kiangazi.

Chanzo: E. Gevorgyan / ZALF

Logo Bundesministerium für Ernährung und Landwirtschaft
Logo Projektträger Bundesanstalt für Landwirtschaft und Ernährung

Kipindi cha mradi: Septemba 2018 – Desemba 2021

Usindikaji na uhifadhi ulioboreshwa kupitia
teknolojia na maarifa.