Kusaidia utengenezaji wa teknolojia za usindikaji ili kuboresha ubora wa virutubishi vya mazao na upatikanaji wa kudumu

Usalama wa chakula na lishe ni moja ya changamoto kubwa kwa watu wengi Kusini mwa Jangwa la Sahara Africa. Upotevu mkubwa wa chakula baada ya mavuno – kwa ubora na kiasi – ni sababu kuu zinazo zorotesha usalama wa chakula na lishe. Sababu za upotezaji mkubwa wa chakula ni uwezo mdogo wa utunzaji wa chakula ambao unaweza kusababishwa na ukosefu wa teknolojia za usindikaji wa kutosha, uwezo wa uhifadhi na maarifa. Ni maendeleo kidogo sana yaliyokwisha patikana katika kuboresha usindikaji na uhifadhi wa jadi wa chakula katika baadhi ya nchi zinazoendelea ambayo yangeweza kutoa mchango mkubwa katika usalama wa chakula na lishe.

Mradi wa Vegi-Leg utafanyika nchi za Tanzania (TZ) na Msumbiji (MS) katika maeneo ya uchunguzi kifani yenye mahitaji makubwa ya lishe ambapo kiwango cha udumavu, upungufu wa damu, na upungufu wa Vitamini A kwa watoto chini ya miaka mitano ni juu ya wastani wa kitaifa. Dhumuni kuu la huu mradi shirikishi wa utafiti ni kulinda usalama wa lishe kwa wakazi wa TZ na MS kwa kusaidia katika utengenezaji wa teknolojia za usindikaji ili kuboresha ubora wa virutubishi vya mazao na upatikanaji wake wa kudumu.

Vegi-Leg italenga matatizo yaliyoainishwa na njia shirikishi yenye kujumuisha wadau mbalimbali kwa kutumia minyororo ya thamani ya chakula kama mfumo wa uchambuzi. Shughuli za mradi zimepangwa katika awamu tatu zinazoshughulikia

  1. ubunifu, uainishaji wa wigo na uchambuzi wa hali halisi
  2. kutengeneza mbinu, majaribio na utekelezaji na
  3. kujenga uwezo na usambazaji (kielelezo namba 1).

Mipango bunifu ya mradi ilipangwa kama sehemu muhimu kuhakikisha usambazaji endelevu wa vyakula vya mimea vilivyosheheni virutubisho kupitia mbinu bora za usindikaji. Mchanganyiko wa teknolojia rahisi kuhakikisha mahitaji ya msingi ya lishe, pamoja na kuwekeza katika teknolojia za usindikaji ili kuongeza thamani kupitia ujumuishaji wa masoko vitatumika kuboresha usalama wa lishe. Mradi wa Vegi-Leg utalenga vyakula vya mimea vilivyosheheni virutubishi Hususan vilivyosheheni protini ya hali ya juu (asidi muhimu ya amino), virutubishi vidogo (chuma) na vimeng’enywa vya mwisho vya mmea (pro-vitamini A carotenoids) na kwa hivyo zilichaguliwa mbaazi (Cajanus cajan) na mboga asilia ya Kiafrika kama mazao kwa ajili ya usindikaji.

Kielelezo namba 1: Awamu tatu za shughuli za mradi wa Vegi-Leg

Kielelezo namba 1: Awamu tatu za shughuli za mradi wa Vegi-Leg

Chanzo: E. Gevorgyan / ZALF