Washirika

ZALF – Leibniz Centre for Agricultural Landscape Research (Müncheberg, Germany)

Wahusika kwa ajili ya mawasiliano:

Dhamira ya ZALF ni kuelezea kisayansi uhusiano sababishi katika mandhari ya kilimo, na kuipa jamii msingi wa maarifa ya matumizi endelevu ya mandhari ya kilimo kupitia utafiti bora. Tofauti na mandhari ya asili, mandhari ya kilimo inategemea matumizi na watumiaji wake. Hivyo basi, utafiti wa ZALF unajumuisha uhitaji wa jamii kwenye mandhari ya kilimo na athari za matumizi yake. ZALF imekuwa ikilenga zaidi utafiti wake juu ya Changamoto kuu za kijamii zinazohusiana na mandhari ya kilimo kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, usalama wa chakula au ulinzi wa viumbe-anuai. Kulingana na kanuni zake, ZALF hutumikia “ustawi wa umma kwa kuwasilisha ufahamu wa kisayansi kwenda sehemu husika za jamii, jumuia za kiufundi na duru za biashara”. Utafiti wa ZALF kiuwazi kabisa unasimamia  ubora wa kisayansi na mwenendo wa uhitaji wa jamii.

SUA – Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (Morogoro, Tanzania)

Wahusika kwa ajili ya mawasiliano:

SUA ni chuo kikuu cha kilimo kinachoongoza nchini Tanzania chenye ndaki tano ambazo ni:  Kilimo, Misitu na Uhifadhi Asili, Tiba na Sayansi ya Mifugo, Sayansi ya kijamii na Sayansi na elimu pamoja na Shule kuu ya uchumi.

Kusudi lake kuu ni kukuza maendeleo kupitia mafunzo, utafiti, ugavi na utoaji wa huduma kwa sekta ya umma na binafsi kwa njia endelevu. Huduma za utafiti, ufikiaji na ushauri zinaendeshwa na kundi la wataalamu wa kilimo na mali asili linalojumuisha wasomi zaidi ya 450, ambao takriban 50% yao wana shahada za uzamivu. Uwezo wa utafiti wa SUA umeimarishwa zaidi kupitia miradi ya utafiti shirikishi, ambayo inasimamiwa  na zaidi ya mikataba 50 ya makubaliano. Mradi wa utafiti uliyokwisha kamilika wa Trans-SEC, uliofadhiliwa na BMBF na BMZ, pia unahusika kwa karibu na SUA. Idara ya Teknolojia ya Chakula, Sayansi ya lishe na mlaji, na idara ya sayansi ya mazao tayari zinashiriki katika miradi iliyofadhiliwa na BMEL.

IIAM – Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Msumbiji
(Maputo, Msumbiji)

Wahusika kwa ajili ya mawasiliano:

IIAM ni taasisi ya utafiti ya umma ambayo inajihusisha na utafiti wa kilimo, maendeleo na huduma za ugavi nchini Msumbiji. IIAM inafanya utafiti, ukuzaji na usambazaji wa teknolojia ya kilimo. Maono ya IIAM ni kuwa taasisi ya utafiti na ubunifu kwa ubora, ambayo inachangia kuhakikisha usalama wa chakula, maendeleo ya biashara-kilimo na matumizi endelevu ya rasilimali asilia. Dhamira ni kutoa suluhishi za kiteknolojia ili kuboresha maendeleo ya biashara-kilimo, usalama wa chakula na hali ya lishe kwa watu wote wa Msumbiji. Malengo makuu ya IIAM ni (i) kukuza tija, kuhakikisha uzalishaji thabiti na uendelevu wa minyororo ya thamani ya mazao makuu (ii) kuchangia katika kuleta ushindani wa mnyororo wa thamani wa zao  kuu unaozingatia mwenendo wa soko, (iii) kuchangia katika usalama wa chakula, lishe na afya, ( iv) kuongeza mwingiliano na ujumuishaji wa IIAM ili kuleta  uendelevu wake wa kitaasisi, (v) kuboresha ustawi wa kijamii na kiuchumi wa wakulima wadogo kwa kuboresha kuongeza thamani ya bidhaa ghafi za kilimo na (vi) ufikiaji wa soko kubwa na fursa za kuboresha mazao ya chakula kwa kukuza usindikaji wa bidhaa za kilimo na uimarishaji wa uhusiano wa soko.

UHOH  – University of Hohenheim (Hohenheim, Germany)

Wahusika kwa ajili ya mawasiliano:

Chuo Kikuu cha Hohenheim (UHOH), kinachojumuisha vitivo vitatu, kinadumisha ushirika wa karibu wa kimataifa na vyuo vikuu na taasisi zingine za utafiti katika nchi zaidi ya 90. Kwa miongo kadhaa, Taasisi ya Kemia ya Baiolojia na Lishe (Prof. HK Biesalski, Profesa Jan Frank) imekuwa ikifanya kazi katika miradi inayolenga nchi zinazoendelea kuboresha hali ya lishe ya makundi yaliyo hatarini na kuchambua virutubishi vidogo vidogo kwenye vyakula na faida zake pamoja na vimelea vyenye faida kiafya vilivyopo kwenye chakula

SIDO – Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (Dar es Salaam, Tanzania)

Wahusika kwa ajili ya mawasiliano:

Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) ni shirika shirikishi la kiserikali chini ya Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko ya Tanzania. Lengo lake kwa jumla ni kuchangia kumaliza umasikini na utengenezaji wa ujasiliamali na hivyo kuchangia maendeleo ya uchumi kupitia utoaji wa huduma zinazolenga uhitaji ambazo zitaleta ajira na kutoa mapato kwa mtumiaji wa huduma. Hivyo basi, dhamira ya SIDO ni kukuza, kuunda, kusaidia na kuendeleza msingi wa ujasiriamali asilia katika tasnia ya viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo. Kazi kubwa ni (i) kusaidia maendeleo ya viwanda vidogo na kupanga na kuratibu shughuli zao, (ii) kutoa msaada wa kiufundi, usimamizi na huduma za ushauri kwa wafanyabiashara wadogo wa TZ na (iii) kusaidia katika utoaji wa miundombinu ya mafunzo kwa ajili ya watu wanaohusika au walioajiriwa au wanao tarajia kuajiriwa katika tasnia ya viwanda vidogo na kusaidia na kuratibu shughuli za taasisi zingine zinazoji shughulisha na mafunzo kama haya.

UniLurio – Universidade Lúrio (Nampula, Mozambique)

Wahusika kwa ajili ya mawasiliano:

Chuo Kikuu cha Lúrio ni chuo kikuu cha kitaifa cha umma na chuo kikuu cha kwanza cha ufundi Kaskazini mwa Msumbiji. Kina makao makuu katika mji wa Nampula na vitivo huko Pemba (mkoa wa Cabo Delgado) na Unango (Niassa), inajumuisha vitivo saba vinavyotoa kozi zifuatazo na zimetawanywa, kwa mtiririko huu a) Kitivo cha Sayansi ya Afya, b) Kitivo cha Usanifu na Upangiliaji wa majengo, Maendeleo Miji na Mipango ya maeneo ya makazi, c) Kitivo cha Sayansi ya Binadamu na Jamii, d) Shule ya Biashara ya UniLúrio, e) Sayansi ya Asili, f) Kitivo cha Uhandisi na g) Kitivo cha Sayansi ya Kilimo. UniLúrio inatoa kozi 23 za shahada ya kwanza na kozi 12 za shahada ya uzamili zinazofikia jumla ya wanafunzi 4000 kwa kuhusisha wahadhiri 330, wengi wao wakiwa wanawake.